Tarehe 29.09.2017 Wanakamati wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Buhigwe kwa kushirikiana na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Wilaya sanjari na Baraza la Waheshimiwa Madiwani walikutana katika ukumbi wa CHAMPANDA wilayani humo kujadili na kupitisha ajenda kuhusu kupanua fursa za biashara na uwekezaji katika Wilaya ya BuhigweMwenyekiti wa KAMATI TENDAJI Baraza la Biashara Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndugu Anosta Nyamoga alifungua Kikao mnamo saa 11:45 asubuhi kwa kuanza na utambulisho wa meza kuu, ambapo aliongoza utambulisho huo kwa kuanza na yeye mwenyewe, kisha mwenyekiti TCCIA (Bw. Azaria Asheri), Meneja LIC-Kigoma (Dr. Betty Mlingi), mwakilishi TNBC ( Bw. Annosisye Mwamsiku), Katibu Tawala Wilaya ya Buhigwe (Ndg. Peter Masindi) pamoja na wajumbe wa kamati tendaji.
Meneja (LIC- Kigoma) alielezea umuhimu wa kujumuisha Baraza la Madiwani na wajumbe wa Baraza la Biashara ili kwamba wajadili kwa pamoja kutatua changamoto zinazokabili ukuaji wa uchumi ndani ya Wilaya. Meneja LIC- Kigoma aliongeza kwamba majadiliano baina ya Baraza la Biashara na Baraza la Madiwani yatafanya mabaraza yawe na nguvu hata mradi wa LIC ukimalizika na Baraza la Biashara liweze kujiendesha lenyewe. Waheshimiwa madiwani watapata fursa ya kujua kinachoendelea kwenye maeneo yao ikiwa ni pamoja na changamoto za kiuchumi zilizopo kwenye kata zao na utatuzi wake.
Kituo cha Biashara (One Stop Business Centre) kilichukuliwa kama mfano ambapo kilionekana kuwa kigeni kwa baadhi ya waeshimiwa madiwani kutokana na kutojua kinachojadiliwa kwenye vikao vya Baraza la Biashara Wilaya na maazimio yake. Hivyo kuletwa pamoja kwa mabaraza hayo mawili ilionekana ni muhimu ili kupisha sintofahamu zinazoweza kuibuka kutokana na kwamba Waheshimiwa Madiwani wachache ndio wanaofahamu uwepo wa Baraza la Biashara la Wilaya.
Agenda zilizo jadiliwa nikama zifuatazo:-
AJENDA 1: UFAFANUZI WA BARAZA LA BIASHARA, MUUNDO WAKE NA MAJUKUMU YA WAJUMBE NA UFAFANUZI JUU YA MRADI WA LIC.
Ajenda hii imegawanyika katika makundi makuu mawili nayo ni yafuatayo:-
BARAZA LA BIASHARA TAIFA (TNBC)
Ni Sekretarieti / Chombo kilicho undwa kwa waraka wa Rais Na.1 wa mwaka 2001 na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 691 - 28 Sept 2001. Kwa lengo la kuboresha mazingira ya Biashara kwa maendeleo ya Taifa.
Kaburasha la ajenda hii limeambatanishwa kwa lengo la kuwapa wajumbe fursa ya kupitia wakati mratibu akifafanua ajenda hii
AJENDA 2: ONE STOP BUSINESS CENTRE.
Meneja mradi wa LIC mkoa wa Kigoma(Dr. Betty Mlingi) alieleleza juu ya kujengwa kwa kituo cha huduma za Biashara cha Wilaya (One Stop Business Centre) na Ufafanuzi juu ya mradi wa LIC.
AJENNDA 3: MAFANIKIO YA BARAZA LA BIASHARA WILAYA YA BUHIGWE
A: UTANGULIZI.
Baraza la Biashara la Wilaya ya Buhigwe liliundwa Tarehe 19.05.2016 na Mwenyekiti wa Baraza na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe wa wakati huo Mhe. Marry Tesha Onesmo. Mwenyekiti wa Baraza hilo aliongea mambo mengi kuhusu umhimu wa mabaraza ya biashara kwa sekta ya Umma na Binafsi katika kutatua changamoto za kibiashara zinazokwamisha ukuaji wa Uchumi katika maeneo husika. Mheshimiwa Mwenyekiti wa Baraza alienda mbali zaidi na kusema mazungumzo ya kirafiki baina ya sekta hizi mbili ndio yanaweza kutatua changamoto mbalimbali za biashara na kuchumi, na kushauri kwamba kuwe na umoja baina ya sekita hizi juu ya utatuzi wa maswala mbalimbali.
B: MAFANIKIO.
Uwepo wa jukwaa la majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.
Uanzishwaji wa baraza la biashara ndani ya Wilaya imeongeza fursa ya majadiliano baina ya sekta ya umma na sekta binafsi. Kabla ya baraza la biashara kuanzishwa sekta binafsi ilikuwa inapata wakati mgumu hasa linapokuja suala la kujadili mambo yanayokwamisha ukuaji wa biashara na upatikanaji wa fursa za uwekezaji Wilayani. Baraza hili limekuwa likiwakutanisha wadau na taasisi za kifedha kama vile NMB kwa lengo la kupata elimu juu ya masuala ya kifedha.
Wajumbe wa baraza la biashara wamejengewa uwezo wa kujenga na kutetea hoja. Kupitia mijadala na mafunzo yanayoendeshwa ndani ya baraza la biashara wajumbe wa sekta ya umma na sekta binafsi wameongeza ufanisi wa kuwasilisha na kutetea ajenda. Ajenda hizo zaweza kuwa ni changamoto zinazokwamisha ukuaji wa uchumi ndani ya wilaya ama ajenda zinazoibua fursa za uwekezaji na uboreshaji wa mazingira ya biashara.
Baraza la biashara limeongeza wigo wa upatikanaji wa elimu juu ya masula ya biashara, elimu ya mlipa kodi, ujasiriamali na uwekezaji.
Ndani ya baraza la biashara elimu ya biashara, mlipa kodi, ujasiriamali na uwekezaji hutolewa. Elimu mojawapo ni kuhusu uhararishaji wa biashara pamoja na mfanyabiashara kuwa na leseni ya biashara, misingi ya uanzishwaji wa biashara ni mambo gani mfanyabiashara inabidi kuzingatia. Baraza limesaidia wafanyabiashara kupata elimu juu ya ulipaji kodi.
Baraza la biashara limesaidia kubaini matatizo yanayoikabili sekta binafsi.
Mijadala inayoendeshwa ndani ya vikao vya baraza la biashara imewezesha kubaini ni matatizo gani ama ni changamoto zipi sekta binafsi inakumbana nazo katika utekelezaji wa shughuli za kiuchumi. Mojawapo ya matatizo hayo ni kama yalivyoainishwa hapa chini:-
AJENDA 4: KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA
Soko la Munanila lilivunjwa mwaka 2004 baada ya serikali kuwa na mpango wa kupitisha barabara ya lami katika eneo la soko la kutoka Kigoma hadi Munanila. Mpango huu wa serikali ulikuwa kuondoa kero au tatizo la usafirishajiwa bidhaa,mazao na abiria kutoka Manyovu hadi Kigoma.
Baada ya kuvunja vibanda vya kudumu 120 vilivyokuwa vimejengwa katika eneo hilo tangu mwaka 2004, hadi sasa hakuna mpango uliowazi wa serikali kufidia vibanda hivyo na kutenga eneo lingine kwa ajili ya ujenzi wa vibanda vya Biashara.
Kwa maana hiyo Halmashauri inaendelea kupoteza mapato ambayo ingepata kutokana na;
KASULU HADI MANYOVU.
Barabara hii ni muhimu kwa kusafirisha abiria ,bidhaa mbalimbali za biashara na mazao ya kilimo. Gharama za usafirishaji katika barabara hii ni kubwa , mfano nauli ya abiria kutoka Manyovu hasi Kasulu ni Tsh 7,000/= (elfu saba). Gharama za usafirishaji zimekuwa juu kwa sababu ifuatayo;
Barabara hii imejaa mawe kiasi ambacho ni hatarishi kwa wenye magari kwa kupasuka tyres na kupasua vioo vya gari.
MUNANILA HADI MWAYAYA.
Barabara hii ni muhimu kwa kusafirisha mazao ya kilimo kutoka Mwayaya,Muhinda na Nyaruboza hadi katika eneo la soko kuu la Munanila.
Barabara hii haipitiki kipindi cha masika ambapo wakulima wanashindwa kufikisha mazao yao soko kuu la Munanila. Vilevile wafanyabiashara wa maeneo hayo hushindwa kusafirisha bidhaa za madukani katika vijiji hivi katika kipindi hiki.
MAONI: Barabara hii itengenezwe kwa kiwango cha Changarawe ili iweze kupitika kwa muda wote.
Zao hili hulimwa katika vijiji vya Kinazi na Janda. Pamoja na hamasa ya kuzalishwa/kulimwa kwa zao hili katika vijiji hivi, bado kuna changamoto ambazo zinarudisha nyuma uzalishaji wake.
Mfano;
Pamoja na hamasa ya kulima/kuzalisha zao hili katika vijiji vya Munzeze, Kishanga na Kigogwe kuna changamoto ambazo zinarudisha nyuma uzalishaji wa zao hili.
Mfano;
MAONI: Halmashauri itafute namna ya kutatua kero hizi kwa ujumla ili wananchi waendelee kuhamasika kuzalisha mazao haya.
Kundi hili lielimishwe mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Mfano;
Kundi hili lielimishwe juu ya mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Mfano;
MAONI: Halmashauri Kwa kuwatumia wataalaamu waliopo ihakikishe makundi haya ya Wakulima na Wafugaji wanaelimishwa kwa kina kuhusu swala la matumizi bora ya ardhi.
ELIMU YA BIASHARA:
Elimu ya biashara ni pana kwa kuzingatia upana huo, leo tutaangazia elimu juu ya leseni za biashara na kadri tutakapo kuwa tunakutana katika maeneo mbalimbali ya wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla tutazidi kujulishana mambo mengi zaidi kuhusiana na elimu ya biashara.
SHERIA YA LESENI ZA BIASHARA NA MAREKEBISHO YAKE (Business Licensing Act No 25 of 1972, Amendment 1980, 2014 and 2015).
Hapa chini ni ufafanuzi wa mambo ya msingi kwa wafanyabiashara na wananchi wanaotarajia kuanzisha biashara mbalimbali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MASHARTI YA KUPATA LESENI YA BIASHARA:
Mtu yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya biashara ili mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu na ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai (katika kipindi cha miezi 12 iliyopita) na awe na eneo la kufanyia biashara linalokubalika kisheria. Kwa mtu ambaye siyo raia wa Tanzania anapaswa kuwa na Hati ya kuishi nchini daraja `A`(Residence permit class A) na nyaraka nyingine za usajili wa kampuni yake ndio aweze kufanya biashara nchini.
Mwombaji anapaswa kujaza fomu ya maombi TFN 211 kikamilifu na kuambatanisha kivuli cha:-
(i) Certificate of Incorporation iwapo ni kampuni na Certificate of Registration and Extract kama ni jina la biashara.
(ii) “Memorandum and Article of Association”ambayo inaonesha kipengele ambacho kampuni hiyo inakiombea leseni ya biashara.
(iii) Passport ya Tanzania au Kitambulisho cha uraia au Kitambulisho cha mpiga kura au Cheti cha kuzaliwa au Hati ya kiapo(affidavit) kuonyesha kuwa ni Mtanzania na Mgeni Hati ya kuishi nchini daraja la “A” (Residnece Permit Class “A”).
(iv) Hati ya kiuwakili (Powers of attorney) Iwapo wenye hisa wote wa Kampuni wapo nje ya nchi,itolewe kwa mtanzania ambaye anaishi hapa.
(v) Ushahidi wa maandishi kuwa ana mahali pa, kufanyia biashara (Kwa mfano hati za nyumba, mkataba wa upangishaji, risiti za malipo ya kodi za majengo au ardhi.
(vi) Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi TRA (TIN).
vii) cheti cha kumaliza (uhitimisho) wa kulipa kodi (Tax Clearence Certificate).
(viii) Kwa leseni zinazodhibitiwa na Mamlaka mbalimbali ,Kwa mfano (TFDA, EWURA,ERB,TPRI,TCRA,CRB,TALA,CAL) n.k lazima mwombaji kuwa na leseni husika kabla ya kuomba leseni ya biashara.
(ix) Hati za utaalam( Professional certificates) kwa biashara zote za kitaalam mfano Ushauri wa kitaalam( Consultancy),udaktari,urubani wa ndege,uhandisi nk.
NB: Ikumbukwe kwamba maombi mapya yanapitia ngazi zote za mwanzo kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kupitishwa au kupatiwa leseni,ambazo ni Afya, Mipango miji na Afisa biashara (W) au eneo ambapo biashara husika inayoombewa leseni itafanyika.
Mtu yeyote anayetenda majawapo ya makosa hapo juu adhabu yake ni faini isiyopungua Tshs. 200,000 na isiyozidi Tshs. 1,000,000 au kifungo kisichozidi miaka miwili (2) au faini na kifungo kwa pamoja.
ANGALIZO: Leseni za biashara hulipiwa ada na kuhuishwa (renew) kila mwaka kwa mjibu wa sheria ya leseni no. 25 ya 1972 na marekebisho yake ya 2014). Mfanyabiashara anatakiwa kuhuisha leseni yake ya biashara ndani ya siku 21 tangu ilipomalizika na penalty ya 25% itatozwa kwa wanaochelewa na itakuwa ikiongezeka kwa 2% kila mwezi.
GS1 Tanzania ni taasisi iliyoanzishwa na serikali kupitia wizara ya Viwanda na Biashara na uwekezaji ikishirikiana na taasisi ya sekta binafsi (TPSF) ikiwa na jukumu la kutoa alama za mistari za misimbomilia (Barcode) na mfumo wa ufuatiliki (Tracebility) kwa bidhaa za Tanzania. Taasisi hii ilisajiliwa na Brella na ilianza kazi zake za utoaji wa alama za utambulisho wa bidhaa Msimbomilia (Barcode)nchini kuanzia tarehe 23 august 2011. Namba ya utambulisho wa bidhaa za Tanzania ni 620. Hivyo Barcode zote za Tanzania zinaanzia na namba 620.
Barcode ni alama za mistari za utambulisho wa bidhaa ambao kila bidhaa inatakiwa kuwa na Barcode yake endapo inatofautiana na nyingine kwa ladha,harufu,ufungashaji,ujazo,umbile,uzito na rangi. Hii inamaanisha kila bidhaa inapotofautiana kwa chochote inapaswa kuwa na Barcode yake.
Bidhaa za Tanzania kukubalika masoko ya nje na ndani ya nchi. Ili bidhaa za Tanzania zikubalike kwenye masoko yaliyo rasmi ni lazima iwe na alama za utambuzi (Barcode).
Ili uweze kupata Barcode kutoka GS1 Tanzania unahitaji kuwa na;
Kwa kufanya hivi GS1 inakuwa inawarasimisha kutoka ufanyaji biashra holela mpaka walio rasmi.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ni shirika la Umma chini ya wizara ya Viwanda na Biashara lililoundwa chini ya Sheria ya Bunge namba 1 ya mwaka 1975 na kurekebishwa chini ya sheria namba 1 ya mwaka 1977.
Mpaka sasa TBS imeshaweka viwango zaidi ya 1600 katika Nyanja za kilimo na chakula, ngozi, kemikali, nguo, uhandisi, mitambo, umhandisi umeme na kadhalika.
TBS huchukua sampuli wakilishi kabla bidhaa hazijapakuliwa katika bandari na mipaka yetu ili kuthibitisha ubora wa bidhaa husika. Bidhaa bora t undo huingia nchini.
Bidhaa zinazoingia nchini kutoka nje ya nchi hukaguliwa katika nchi zinakotoka kabla kusafirishwa kuja nchini.
KWA MTEJA/MLAJI:
KWA MZALISHAJI:
Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) ni taasisi iliyo chini ya wizara ya Afya na ustawi wa jamii yenye jukumu la kudhibiti ubora na usalama wa vyakula,dawa ,vipodozi na vifaa tiba.
TFDA imeanzishwa chini ya sheria ya chakula,dawa na vipodozi ,sura 219 na ilianza kutekeleza majukumu yake rasmi tarehe 1 Julai, 2003.
Mamlaka hii imejizatiti katika utoaji huduma bora ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja wake kwa kuhakikisha ubora,usalama na ufanisi wa vyakula,dawa, vipodozi na vifaa tiba.
Hivyo wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara za uuzaji wa vyakula, vipodozi, na maduka ya dawa ni vizuri wakajisajili katika mamlaka hii ili kuhakikisha na kuuza bidhaa bora bila matatizo yoyote. Hii itaepuka uuzwaji wa bidhaa zilizoisha muda wake. (Expire) na kusababisha matatizo kwa mlaji/mtumiaji. Kwa kufanya hivyo kwa pamoja tutapambana na bidhaa duni na badia ili kulinda afya zetu.
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ni taasisi ya serkali iliyo na jukumu la kukusanya kodi ya serkali. Kila mwananchi anawajibika kulipa kodi kwa serkali iwe moja kwa moja hasa wafanyabiashara (Direct Tax) ama kwa kununua bidhaa iliyokwisha kamilika kwa ajili ya matumizi (Indirect Tax).
Mfanyabiashara anatakiwa kusajiliwa na mamlaka ya mapato ili kulipa kodi na usajili ukikamilika anapewa namba ya utambulisho wa mlipa kodi (Tax Identification Number – TIN) baada ya zoezi hilo atafanyiwa tathimini kulingana na biashara yake. Mfanyabiashara akilishafanya malipo atapewa cheti cha kumaliza kulipa mapato (Tax Clearence Certificate).
Mwananchi ambaye sio mfanyabiashara analipa kodi kutokana na vitu anavyo nunua kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, kila unaponunua bidhaa yoyote kuna kiasi cha kodi kinakuwa kiko kwenye bidhaa hiyo.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz