Kitengo cha Tehama
Kitengo cha TEHAMA, na Mahusiano
Kitengo cha (TEHAMA) kimeanzishwa mwaka 2010 kwa kuunganisha kitengo cha Teknolojia ya Habari Mawasiliano na Mahusiano . Kitengo hiki kinaongozwa na Sera ya TEHAMA (2003), na Sera ya Utangazaji Habari (2004). Ibara ya 18 yakatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
SERA YA TEHAMA WILAYA YA BUHIGWE
Idadi ya Watumishi:
Kwa sasa kitengo cha TEHAMA kina watumishi watatu, mmoja mwenye ajira ya kudumu na wawili ni ajili ya muda.
Kama unahitaji msaada wa kitaalamu kutoka kitengo cha TEHAMA wasiliana na Mkurugenzi Mtendaji(W) kisha atakuunganisha na mtaalamu mmojawapo wa TEHAMA.
Kitengo hiki kinasimamia na kuratibu matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, na kutoa usaidizi wa kiufundi kwa mfumo jumuishi wa Kompyuta na mifumo mingine pamoja na Vifaa vya TEHAMA.Aidha, Kitengo kinatoa huduma za kitaalamu kuhusiana na matumizi ya TEHAMA kama ifuatavyo;
a) Kushughulikia utekelezaji wa Sera ya Serikali Mtandao, miongozo, kanuni na viowango vya matumizi na utekelezaji wa TEHAMA.
b) Kuweka mifumo na mitandao ya Serikali Mtandao.
c) Kutoa msaada wa matumizi sahihi ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
d) Kuhakikisha vifaa vya TEHAMA vinahudumiwa kiufundi na kwa wakati..
e) Kutoa msaada wa kiufundi na utaalamu wa kununua Vifaa na Mifumo ya TEHAMA .
f) Kuhudumia na Kuhuisha mifumo na miundombinu ya mawasiliano (LAN/WAN).
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz