Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Siro leo tarehe 12 Disemba 2025 amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.

Katika ziara hiyo ametembelea miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa Wilaya humu ikiwemo mradi wa tenki la maji wa Munanila-Nyakimue wenye uwezo wa kuzalisha maji lita Milioni 8 kwa siku na chemichemi iliyopo katika kijiji cha Munyegera yenye uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita zaidi ya Milion 2.

Akizungumza na baadhi ya wananchi wa Buhigwe amewapongeza kwa kuwa na chanzo kizuri na cha kipekee zaidi chenye utoaji wa huduma ya maji bila ya uhakika.
Aidha ameongezea kwa kuwapongeza Wananchi kwa utunzaji mzuri wa mazingira katika chanzo hicho na maeneo yote.

Miradi hiyo itaongeza huduma ya upatikanaji wa maji kwa Wilaya ya Buhigwe kutoka asilimia 84.3 ya sasa hadi kufikia asilimia 90.1.

Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz