Hospitali ya wilaya ya Buhigwe inatarajia kuanza huduma zake za awali ifikapo tarehe 8/6/2020 haya yamezungumzwa na mganga mkuu wa wilaya (Dk Julias Nyasongo) huku akionesha ni kwa jinsi gani Majengo ya hospitali hiyo yamekamilika .
Pia Mganga mkuu wa wilaya anapenda kuwakaribisha wananchi wote wa wilaya hiyo katika hospitali hiyo huku akitoa shukrani zake za dhati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Bwana Anosta Nyamoga , pia na kwa waziri wa Tamisemi kwa kufanikisha mradi huu mkubwa wa Hospitali ya wilaya ,pamoja na serikali ya awamu ya tano kwa ujumla wake kwa kazi nzuri inayoifanya.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz