Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buhigwe Ndug Hamza Seif Mnaliwa amewaasa Wasimamizi na wasimamizi wa vituo jimbo la Buhigwe kufanya kazi kwa uzalendo na weledi.
Ameyasema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya makarani waongoza wapiga kura,wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa vituo yaliyoanza tarehe 25 oktoba na kufungwa leo tarehe 27 Oktoba 2025.
”kwa niaba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi napenda kuwashukuru na kuwapongeza wote mlioteuliwa kwa nafasi za makarani waongoza wapiga kura,wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa vituo na napenda kuwasihi kutekeleza majukumu yenu mnapokuwa katika vituo kwa uzalendo na weledi”alisema Mnaliwa

Aidha ameongezea kuwahimiza kutunza vifaa watakavyokabidhiwa na kuvitumia ipasavyo na kuhakikisha mabango yanabandikwa kwa usahihi ili kuepuka ukiukwaji wa masharti ya sheria na kanuni za uchaguzi.

Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz