Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdory Mpango leo tarehe 29 Oktoba 2025 amewaasa Watanzania wote Nchini kuiga mfano wa wananchi na wakazi wa kijiji cha Kasumo Wilayani Buhigwe wa kwenda mapema kupiga kura kuchagua Rais,wabunge na Madiwani.

Akizungumza baada ya kupiga kura katika kituo cha kijiji cha Kasumo,kata ya Kajana Wilaya ya Buhigwe amewapongeza Wananchi waliojitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.

Sambamba na hilo ametoa wito kwa wengine ambao bado hawajenda kupiga kura kujitokeza kwa wingi kama walivyofanya wakazi wa kijiji hicho.


Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz