Wahandisi wa miundombinu wilayani Buhigwe wametakiwa kusimamia na kufuatilia kwa makini miradi inayotekelezwa katika Wilaya hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati.

Tamko hilo limetolewa leo tarehe 7 Novemba 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina wakati akikabidhi pikipiki kwa Wahandisi hao kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali.

Aidha ameongezea kwa kumpongeza Mkurugenzi mtendaji Ndug George Emmanuel Mbilinyi na Menejimenti ya Halmashauri kwa kuwezesha upatikanaji wa pikipiki hizo 8 za aina ya Boxer Bajaji ambazo kiasi cha shilingi Milioni 30 kimetumika kununua
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz