Halmashauri ya wilaya Buhigwe inataraji kupokea mbio za mwenge wa Uhuru mnamo tarehe 23/07/2017. Na kuzungukia miradi ya maendeleo katika wilya ya Buhigwe. Miongoni ya miradi itakayo pitiwa na Mwenge wa Uhuru ni pamoja na
Moja ya shughuli zitakazo fanyika wakati wa mwenge ni kukagua miradi hiyo pamoja na kutoa elimu kwa jamii juu ya taarifa za maendeleo katika jamii ya Wilaya ya Buhigwe na Tanzania kwa ujumla.
Kwa kujiandaa na hili Mkuu wa wilaya Buhigwe Con. Marcos Gaguti akiongozana na Mkurugenzi mtendaji (W) Buhigwe Bwa. Anosta Nyamoga pamoja na baadhi ya wakuu wa idara wenye miradi walipitia miradi iliyochaguliwa na ambayo itapitiwa na mwenge.
Njia iliyopendekezwa ya mwenge itakuwa kama ifuatavyo (Kwataarifa za awali)
Lengo kuu na ziara hii ya ukaguzi wa njia ya mwenge ni kujiridhisha kwamba miradi yote iliyopendekezwa na wakuu wa idara ifikia kiwango au kuwa na sifa za kutembelewa na mwenge huo.
I. Mwenge wa Uhuru umekuwa ni chombo muhimu cha kujenga undugu, umoja, mshikamano na kudumisha amani pote unapopita bila kujali itikadi zetu za kisiasa, dini wala makabila yetu. Umuhimu huu unatokana na ukweli kwamba, leo hii tunahitaji kujenga Taifa lenye amani, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa kuliko wakati wowote ule ikiwa ni pamoja na kujenga taifa lisilokuwa na dhuluma, unyonge, rushwa, ubaguzi, ukabila, udini wala vitendo vya kifisadi.
II. Mbio za Mwenge wa Uhuru zimeendelea kuhamasisha wananchi kwa kushirikiana na Serikali yao katika kubuni na kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo katika nyanja za kilimo, ufugaji, Uvuvi endelevu, uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya, elimu, maji, umeme na huduma za jamii katika maeneo yote nchini na hasa katika maeneo yasiyofikika kiurahisi.
III. Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa zikitumika kuelimisha wananchi katika maeneo yote nchini jinsi ya kupambana na maradhi yanayotishia ustawi wa watu wetu kama vile UKIMWI, Malaria na kupambana na matumizi ya Dawa za kulevya. Pamoja na njia nyingine tunazotumia kuwahamasisha wananchi wetu. Bado Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa ni njia sahihi ya kufikisha taarifa na elimu sahihi ya changomoto hizi kwa watanzania wote.
IV. Mbio za Mwenge wa Uhuru pia, zimeendelea kuhamasisha na kuimarisha umuhimu wa Muungano kwa watanzania wa pande zote mbili za nchi yetu.
V. Kimataifa, Mwenge wa Uhuru umeendelea kusimamia dhana ya na maudhui yake ya kumulika hata nje ya mipaka yetu. Kwani umeendelea kuhamasisha amani ndani ya Afrika Mashariki, Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika na Duniani kwa ujumla. Tanzania imeendelea kuwa msuluhishi wa Amani Afrika na mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine Duniani kote na imeshiriki ukombozi wa Bara la Afrika hasa kusini mwa Afrika na kusisitiza juu ya umoja, mshikamano, upendo na amani kwa mataifa hayo.
VI. Mwenge wa uhuru umeendeleza falsafa ya kumulika ndani ya mipaka ya taifa letu kwa kumulika uovu katika jamii ikiwemo uzembe, kutowajibika, vitendo vya rushwa na ufisadi katika miradi mbalimbali ya maendeleo na huduma za kijamii nchini.
VII. Mbio za Mwenge wa Uhuru pia hutumika katika kuratibu na kutathimini shughuli mbambali za maendeleo zinazofanywa na wadau wa maendeleo na kukusanya taarifa zinazohusu kero za wananchi ambazo husaidia Serikali katika upangaji na utelezaji wa mipango ya maendeleo kwa wananchi wake.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz