Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Col MICHAEL MASALA JUSTIN NGAYALINA ameongoza zoezi la upandaji miti katika eneo la Halmashauri lenye ukubwa wa hekari 2 zaidi ya miti 1000 aina ya mkuyu ambayo ni rafiki wa maji imepandwa ikiwa ni maadhimisho ya siku ya misitu Duniani na upandaji miti kitaifa kauli mbiu ni ``Msitu na Ubunifu"
Zoezi hilo la upandaji miti limefanywa na watumishi wote wa Halmashauri kwa kushirikiana na kikundi Cha songambele kiitwacho street knowledge ambacho kinajihusisha na utunzaji wa mistu na ujasiriamali mdogo mdogo.
Mh Mkuu wa wilaya amewashukuru na kuwapongeza watumishi wote na kikundi hicho kwa Ushirikiano wao waliouonesha katika zoezi hilo kwa kusema kuwa waendelee na moyo huo huo wa kujitolea kushiriki kazi za Halmashauri ili twendelee kuifanya buhigwe ing'are zaidi na zaidi
Pia zoezi la upandaji miti kwa buhigwe ni endelevu ili kuhakikisha tunapata misitu ya kutosha kwaajili ya kulinda vyanzo vya maji na mmomonyoko wa aridhi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz