Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George Emmanuel Mbilinyi ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza miradi mbalimbali katika Wilaya hii kuhakikisha miradi yao inawanufaisha wananchi kiuchumi.

Ameyasema hayo leo tarehe 19 January 2026 wakati akizungumza na mashirika hayo katika ofisi za Halmashauri hiyo.
Aidha ameongezea kwa kuwasihi kufanya kazi kwa ushirikiano na kutanguliza uzalendo mbele katika shughuli zao.
Sambamba na hilo amewataka kufanya kazi kwa weledi na kwa wakati uliokusudiwa ili kuleta tija katika maisha ya Watanzania.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz