Wakulima wa kahawa katika Wilaya ya Buhigwe wamehimizwa kuchangamkia fursa katika sekta ya kilimo kwa kupanda mbegu mpya ya zao la Kahawa.
Akizungumza na Wakulima wakati wa zoezi la ugawaji wa miche ya kahawa katika kitalu cha Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI) kilichopo katika Kijiji cha Mwayaya Wilayani hapa, Kaimu Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilayani Buhigwe Mhandisi Mjairi B. Julius amewahimiza wakulima kupanda miche hiyo kwenye mashamba yaliyoandaliwa kitaalamu na kuzingatia nafasi kati ya mche na mche.
Aidha kwa wakulima ambao bado wana miche mikuukuu amewashauri kuing’oa kwa awamu huku wakiendelea kupanda miche mipya ambayo inazaa kwa wingi na haishambuliwi na magonjwa kwa urahisi.
“Kwakuwa kitalu hiki kimeoteshwa katika kijiji chenu hakikisheni mnachangamkia fursa ili kujiongezea kipato na kujikwamua kwenye wimbi la umaskini pia epukeni kuzurura ovyo mitaani na vijiweni badala yake fanyeni kazi ili kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sera ya “Hapa kazi tu”, alimazia Kaimu Afisa Kilimo na kuwashukuru wakulima waliojitokeza katika zoezi hilo.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz