Mkuu wa Mkoa Kigoma Mhe. Brig. Generali Mstaafu Emmanuel Maganga ameendesha zoezi la utoaji vitambulisho kwa wazee wasiojiweza kutoka kata 10 za Wilaya ya Buhigwe.
Zoezi hilo limefanyika leo asubuhi katika kijiji cha Mwayaya.
Akizungumza na Wazee hao Mhe. Mkuu wa Mkoa amewaasa kuvitumia na kuvitunza Vitambulisho hivyo kwa ajili ya kupata matibabu bure katika Zahanati, Vituyo vya Afya na Hospitali zote za Mkoa wa Kigoma.
Aidha amewakemea Wananchi wanaowaua Wazee kwa imani za kishirikina, kuwakatili na kuwatelekeza wazee na yeyote atakayebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho aliwaomba Wananchi kwa ujumla kuondokana na janga la kuchoma moto kwani ni uharibifu wa mazingira na kuwahimiza kujenga utaratibu wa kupima Afya zao na kujiunga na Bima ya Afya.
KAULI MBIU;" Kuelekea Uchumi wa Viwanda, Tuthamini mchango, uzoefu na ushiriki wa Wazee kwa Maendeleo ya Taifa letu"
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz