Ni lazima wazazi washirikiane kuhakikisha mtoto ananyonya maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo bila kulishwa au kunyweshwa kitu chochote,Aidha mtoto anyonye maziwa ya mama kwa muda usiopungua miaka miwili. Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Buhigwe Ndg. Peter N. Masindi, mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika katika viunga vya zahanati ya kijiji cha Kibwigwa leo asubuhi.
Kwa upande wake Mratibu wa afya ya mama na mtoto Wilaya ya Buhigwe Bi. Saverina Kyeshe amesema kuna faida nyingi sana za unyonyeshaji kwa mama, mtoto na familia kwa ujumla. Nawasisitiza akina mama wa Wilaya ya Buhigwe kunyonyesha watoto ili kuwakinga watoto dhidi ya magonjwa mbalimbali kama kuhara, utapiamlo, kupungua uzito, udumavu na hata vifo, pia faida kwa akina mama ni pamoja na kutokupata hedhi na hivyo kuzuia mimba kwa kipindi cha miezi 6 ya mwanzo, kuepuka magonjwa ya kuvimba chuchu au matiti, na kupunguza uwezekano wa kupata fistula. Alisema Saverina.
Afisa Lishe(w) Bi Theodora Thomas alisema maziwa ya mama ya njano ni muhimu sana kwa afya ya mtoto, baadhi ya akina mama huyakamulia chini kwamba ni machafu kitu ambacho ni imani potofu inayopaswa kupigwa vita. Hakuna mama ambaye maziwa yake ni machafu, maziwa ya mama yoyote yana virutubisho sawa tuache dhana potofu tubadilike. Alisema Theodora.
Aidha Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Ndg. Notas Makuna alimalizia kwa kusema "Malengo yetu ni kuhakikisha elimu hii ya unyoyeshaji inawafikia wananchi wote wa Wilaya ya Buhigwe".
Mwisho natumia fursa hii kuwashukuru wananchi wote mliohudhuria maadhimisho haya. Kibwigwa oyeeeee!!!!!!!!.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz