Akizungumza na watendaji wa vijiji na kata na mawakala wanaokusanya mapato wa halmashauri hiyo katika kikao kazi kazi leo Julai 30, 2021 katika ukumbi wa halmashauri, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo aliyewakilishwa na Afisa Uchaguzi alisema Pamoja na majukumu mengine watendaji hao waliyonayo bado wana jukumu zito la kuongeza na kusimamia mawakala wanaokusanya mapato kwenye maeneo yao.
Muwakilishi(kushoto aliyekaa) wa Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya na menejimenti wakisikiliza kero na changamoto za watendaji wa kata na vijiji Pamoja na mawakala wa kukusanya mapato leo Julai 30 katika kikao kazi kwenye ukumbi wa halmashauri.
Ameongeza kuwataka kujituma na kujitoa kuona kuwa mapato ya halmashauri yanapaa.
Katika kikao kazi hicho nyeti kwa mustakabali wa halmashauri watendaji na mawakala walipata nafasi ya kutoa changamoto na matatizo yao na kujibiwa na kupata ufumbuzi wa menejimenti.
Pia kila Kijiji na kata vilipangiwa kiwango cha ukusanyaji kwa mwaka na kwa mwezi ili kufikia lengo lililowekwa.
Kikao kazi hicho kilihitimishwa kwa mkuu wa idara ya Utumishi na Utawala ndg. Idrisa Kuwataka watendaji hao kurejea kwenye muundo wa utekelezaji wa majukumu yao na kujitoa pasipo mipaka kwa kuwa ofisi yake kamwe haitovumilia uzembe na uvivu kazini.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz