Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi 2025 ngazi ya kata jimbo la Buhigwe leo tarehe 04 mwezi Agosti 2025 wameapishwa na Hakimu mkazi Mfawidhi Mahakama ya mwanzo Wilaya ya Buhigwe Mh Straton Mosha wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wasimamizi hao.
Mafunzo hayo ni ya siku tatu kuanzia tarehe 04 hadi 06 mwezi huu Agosti yakiwa na lengo la kuwafundisha jinsi ya kuratibu na kusimamia shughuli za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Akizungumza Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Buhigwe Hamza Seif amewataka wasimamizi hao kuwajibika ipasavyo ili kukamilisha zoezi la Uchaguzi kwa Amani na utulivu.
Sambamba na hilo amewasihi kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu na kuzingatia maelekezo wanayopewa na tume huru ya Uchaguzi
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz