Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Buhigwe Ndugu George Emmanuel Mbilinyi amewaapisha Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Wilaya ya Buhigwe na kuwataka kuzingatia maagizo na maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Akizungumza katika Semina kwa Wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi Wilaya ya Buhigwe ambayo imefanyika leo tarehe 30 mwezi Septemba amewasihi kuwa makini katika utekelezaji wa jambo la Uchaguzi ikiwemo kutunza vifaa vitakavyotumika.
Sambamba na hilo amewashauri kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufanikisha zoezi la Uchaguzi kwa maendeleo ya Taifa.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 utafanyika tarehe 27 mwezi Novemba ukiwa na kaulimbiu inayosema “Serikali za Mitaa,Sauti ya Wananchi,Jitokeze kushiriki Uchaguzi”
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz