Wananchi wanaonufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, TASAF wa Wilayani Buhigwe, Mkoani Kigoma wamewekeza Nguvu katika kupanda Miti ili kurudisha Mazingira kwenye Hali yake ya asili.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Ekari zaidi ya 6 za Miti zinazotunzwa na Wanufaika hao, Mhe. Michael Ngayalina amewataka wananchi hao kuendelea na Tabia hiyo si kwa Miradi ya Pamoja bali hata majumbani na kwenye mashamba yao wawekeze katika kupanda na kutunza miti kwa kuwa Faida zake ni nyingi ikiwepo kujipatia Fedha. Hayo yamejiri huko kwenye Kata ya Rusaba wilayani hapo pamoja na Kata ya Kibwigwa
Kwingineko huko kwenye Kata ya Munyegera, Wananchi wa wanaonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, TASAF wamekamilisha Mradi wa Kurekebisha Barabara ya Mtaani yenye Kilometa 4.3 kwa vifaa kama Majembe, Mafyekeo, Mapanga ambapo Mkuu wa Wilaya Hiyo DC Ngayalina amepongeza Ubunifu huo ambao umepunguza adha za usafiri kwenye Barabara hiyo muhimu na kiungo cha Vitongoji Katani Hapo.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz