Wananchi wa Wilaya ya Buhigwe wameaswa kufanya kazi kwa bidi ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuleta maendeleo kwa jamii.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Kibande wilayani Buhigwe Mkuu wa Wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe leo tarehe 26 Novemba 2025 wakati wa kukabidhi soko la Kibande lililojengwa kwa ufadhili wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) kwa kushirikiana na baraza la Wakimbizi la Denmark (DRC).

“kupitia ujenzi wa soko hili ambalo naamini litaongeza kasi ya biashara basi wananchi sasa tupige kazi kuhakikisha tunajikwamua kiuchumi”alisema Kanali Mwakisu

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuari ya Wilaya ya Buhigwe ndug George Emmanuel Mbilinyi ameyashukuru mashirika hayo ambayo yamekuwa yakiisadia Serikali kuleta maendeleo kwa jamii kwa kujenga miundombinu na kuleta miradi mbalimbali ambayo yana matokeo chanya kwa jamii.

Ameongezea kwa kuwasihi wananchi wanaoishi mipakani kudumisha Amani na upendo iliopo baina ya wao na wanaotoka nchi za jirani ikiwemo Burundi na maeneo mengine.
Andrew Chingole ambae ni mwakilishi wa UNHCR, amewaasa kuenzi na kuheshimu juhudi za serikali na mashirika hayo kwa kutunza miundombinu mbalimbali ya soko hilo.
Kwa upande wake mwakilishi wa baraza la Wakimbizi (DRC) Ally Mnari amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa kutoa ushirikiano wa hali na mali kufanikisha ujenzi wa soko hilo.
Kwa niaba ya wananchi wa kata ya Kibande ndug Elia ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuleta maendeleo katika kata hiyo na Wilaya kwa ujumla.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz