Walimu wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma wametakiwa kuacha kufundisha kwa mazoea na badala yake wahakikishe wanawapa watoto ujuzi na si kuharakisha kumaliza mada ili kupandisha kiwango cha ufaulu.
Rai hiyo imetolewa leo Jumatatu Juni 3, 2024 wilayani Buhigwe na Naibu Katibu Mkuu OR TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde alipokuwa akionge na walimu hao katika ukumbi mkubwa wa Halmashauri.
Amesema ili kufanikisha mkakati wa serikali wa kuongeza ufaulu ni lazima wazingatie misingi minne ya ufundishaji inayojumuisha uwezo alionao mtoto, mazingira wanayopatia elimu, umri waliokuwa nao ili ujue unaenda nao vipi pamoja na utayari wa kupokea unachokitoa kwao.
“F yoyote ni ya mwalimu si mwanafunzi KPI ya kila mwalimu ni kuhakikisha kwenye somo lako hakuna F…ukiangalia ukaona walimu waliokutangulia wamefanya makosa rekebisha kwa kufanya hivyo hawataona kile unachowafundisha ni kigumu,".
Aidha, ameelekeza walimu wa shule za sekondari kuhakikisha wanafunzi wanapojiunga na kidato cha kwanza wanawajengea ujuzi wa kujua lugha ya kiingereza kwa kuandika, kuzungumza, kuelewa na kusoma alafu mchakato wa kuufundisha masomo mengine ndio uendelee.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Emily Fwambo amesema kuwa halmashauri itahakikisha inatekeleza yale yote waliyoagizwa ili kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu na matokeo yake yataonekana.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz