Wamiliki wa vyombo vya habari na waandishi wa habari mkoani kigoma wametakiwa kushirikiana na jamii katika kukuza Kiwango vya elimu mkoani hapo.
Kikao hicho kilihisisha wamiliki wavyombo vya habari, maafisa mawasiliano serikalini, maafsa elimu ngazi ya mkoa na waandishi wa habari waliop mkoani hapo.
Wadau hao wa habari wametakiwa na katibu tawala msaidizi idara ya elimu mkoa wa kigoma bi paulina ndigeza akimuwakilisha katibu tawala wa mkoa huo katika kikao kilichofanyakia katikaukumbii wa groness hotel uliopo halimashauri ya kasulu mji
Katika kikao hicho kiongozi huyo aliwataka wadau wa vyombo vya habari kuendelea kutoa taarifa na elimu kwa umma juu ya mradi inayotekelezwa mkoani hapo ikiwamo mradi wa shule borapia amewataka kuelimisha jamii kushiriki kwa kuzifanya shule ziwajibike na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kila watoto wenye ulemavu kuwaandikishana khudhuria shuleni
Aidha amesema tayari maafisa mawasiliano serikalini kwa ngazi ya mkoa na halimashauri inayotekeleza mradi wa shule bora wamefanya vikao na kuweka maazimio namna watakavyofanya kazi na wamiliki wa vyombo vya habari pamoja na waandishi wa habari katika kuboresha utoaji wa taarifa za mafanikio.
Hata hivyo katika utekelezaji wa mradi wa shule bora wajibu wa wamiliki w avyombo vya habari na waandishi wa habari ni kuibua changamoto na uelimishaji wa jamii katika maeneo yanotekelezwa na mradi ikiwemo suala la ufundishaji mazingira salama ya kujifunzia , elimu jumushi ufaulu na mdondoko wa wanafunzi
Kama mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini ofisi ya raisi tamisem ndugu fred kibano aliwataka waandishi wa habari kutumia kanuni zao kufikisha ujumbe kwa jamii kupitia uandishi wa habari makala uandaaji wa vipindi kupitia vyombo vya habari ikiwemo magazeti radio televisheni na mitandao ya kijamii ili kufikisha ujumbe kwa makundi mbalimbali
Mradi wa shule bora unatekelezwa katika mikoa tisa nchini Tanzania ukihusisha halimashauri sitini na saba na shule elfu tano mia saba hamsini na saba (5757) na unatarajia kunufaisha wanafunzi zaidi ya milioni tatu laki nane (3,800,000)na walimu zaidi ya elifu hamsini na nne (54,000)
Mikoa inayotekeza mradi wa shule bora ni pamoja na mkoa wa kigoma, katavi, Dodoma,mara, pwani, rukwa, simiyu, singida, na mkoa wa mkoa wa tanga
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz