Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe amefanya Kikao na Viongozi wa dini na Wazee Maarufu wa Wilayani humo kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Akizungumza katika kikao hicho amewasisitiza viongozi hao kuhusika moja kwa moja katika zoezi la uhamasishaji wa Wananchi kujiandikisha na kupiga kura ifikapo tarehe 27 mwezi Novemba.
Kwa upande wao Imamu wa Msikiti wa Buhigwe,Jumanne Kwiha na Mchungaji Kiongozi Anglikana Buhigwe Leonard Fedia kwa pamoja wamempongeza na kumshukuru Mkurugenzi kwa kuona umuhimu wao na kuamua kufanya kikao hicho ambacho kimewapa Elimu na namna bora ya kuongea na Waumini wao namna bora ya kuchagua viongozi bora.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz