DC azindua mgao wa ruzuku wa cash plus VIJARUNGA WANG'ARA NA MAMA SAMIA
Mhe Col.Michael M.Ngayalina Mkuu wa wilaya Buhigwe amezindua mgao wa Ruzuku Kwa vijana wa Cash plus Buhigwe. Hata hivyo ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na mama shupavu kweli kweli kwa kutambua na kuthamini nguvu kazi ya vijana. Sio hivyo amewaasa vijana kujikinga na mambo hatarishi kama mahusianao hatarishi, mimba za utotoni na maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Akielezea kuhusu manufaa na lengo la mradi huo Afisa Ufatiliaji wa mpango wa Tasafu amesema Mradi huu wa ‘Cash Plus’ unahusu Ustawi na Mabadiliko Salama Yenye Afya kwa Vijana nchini Tanzania, kwa ufupi “Ujana Salama”, unalenga kuimarisha maisha ya vijana wa vijijini. Vijana hawa wa umri wa balehe wanatoka katika kaya maskini na wanakabiliwa na hatari nyingi za kiafya na kiuchumi. Mpango huo unawalenga vijana wa umri wa balehe miaka Kati ya 14 Hadi 19 katika kaya zinazonufaika na --Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (ruzuku inayojumuisha uhawilishaji pesa, Ujenzi au ukarabati wa miundombinu na kuimarisha njia za kujiingizia kipato katika kaya). Msaada wa kiufundi unatolewa na UNICEF. Vijalunga hao kila mmoja Amepokea Tsh 186,400 Kwa kuandika maandiko ya biashara watakazozitekeleza kwenye maeneo Yao huko vijijini.
Akiongea na Vijana Bi. Utefta Mahega Katibu Tawala wa Buhigwe amewakumbusha kuwa bahati haiji mara mbili na kuwaomba waweke juhudi kubwa katika kutekeleza maandiko waliyoandika ili kuwa na matumizi sahihi ya fedha na kufanya vijana kusonga mbele na kujikwamua na umasikini
Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi amesema hakuna kitu kinafanywa na serikali bila kuwekwa kwenye mikakati hivyo amesema serikali ya awamu ya sita inatekelezaji ahadi ilizozitoa. Hata hivyo amewasihi vijana kutumia ujana wao vizuri ili kuwa na kesho iliyo njema kwao na kujikwamua na umasikini
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz