Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe wajitokeza kufanya usafi kwenye maeneo yanayozunguka office na nje ya office zote za Halmashauri.
Akiongoza zoezi la usafi Kaimu Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug Alphonce Innocent Haule amewasisitiza watumishi wote kufanya usafi sio tu katika mazingira yanayoizunguka ofisi ya halimshauri bali hata majumbani kwetu lengo ni kujikinga na magonjwa ambukizi haswa ya mlipuko ukizingatia msimu huu ambao mvua ni nyingi sana.
Washiriki katika usafi huo ni wakuu wa division na vitengo na watumishi wote waliopo chini Yao huu ni mwendelezo wa kuhakikishia tunaweka mazingira yote yanayoizunguka Halmashauri kuwa safi wakati wote ili kuepusha magonjwa ya milipuko na mazalia ya mb’u pia kutokomeza malaria.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz