Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe ndugu Anosta Lazaro Nyamoga akishirikiana na Mganga mkuu wa wilaya Dkt. Julius Nyasongo wanapenda kuwatangazia wananchi wote wa wilaya ya Buhigwe kujikinga na ugonjwa hatari wa CORONA ambao unaendelea kuua mamia kwa maelfu ya watu duniani.
"Tumuunge mkono Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli na serikali ya awamu ya tano kwa kuchukua tahadhari zote ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu hatari" Alisema Nyamoga.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa wilaya Dkt. Nyasongo alitoa elimu kuhusu ugonjwa huu kwa kueleza chimbuko lake, dalili, namna unavyoenea na jinsi ya kujikinga.
Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyosababisha maradhi kwa wanyama na binadamu. Kwabinadamu, jamii kadhaa za virusi vya Corona vinafahamika kusababisha maambukizikwenye njia ya hewa na mfumo wa upumuaji. Kirusi cha Corona kilichogundulika hivi karibuni kinasababisha ugonjwa unaofahamika kama COVID-19.
COVID-19 ninini?
COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona. Virusi hivyo vipya havikuwa vikifahamika hapo kabla na sayansi ya tiba. Na vilianzia nchiniChina mwezi Disemba mwaka 2019.
Dalili zaCorona ni zipi?
Dalili kuuza Corona ni pamoja na;
1. Homa kali,
2. Uchovu na
3. Kikohozi kikavu
4. Kupumua kwa shida
5. Maumivu makali ya kichwa na zinatokea taratibu. Dalili kubwa na inayoweza kutia hofu, ni mtu kukosa pumzi.
Virusi vya Corona vinasambaa vipi?
Unaweza kupata Virusi vya Corona kutoka kwa watu walioambukizwa. Virusi vinaweza kusambaa kupitia maji maji kutoka kwenye pua au mdomo wa aliyeathirika. Iwapo mtu anagusa maji maji kama mafua, mate na makohozi ya mtu aliye na virusi na kisha kujigusa mdomo, macho na pua anaweza kupata virusi vya Corona.
Ninaweza kujikinga vipi na Virusi vya Corona?
Alihitimisha kwa kutoa rai kwa wananchi wa wilaya ya Buhigwe na watanzania wote kwa ujumla kutopuuza tamko la serikali kuhusu ugonjwa huu.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz