Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Col. Michael Masala Ngayalina amelaani vitendo vya uchomaji moto vinavyofanywa na baadhi ya wananchi waliokosa uzalendo na urafiki wa mazingira. Nawaomba wananchi wenye mapenzi mema tushirikiane katika kutokomeza tabia hii mbaya. Endapo mtu atabainika kwamba amehusika katika kuchoma moto akamatwe na kupelekwa kwenye vyombo vya dola ambapo atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufungwa jela, kutoa faini au vyote kwa pamoja. alisema Mhe. Ngayalina alipotembelea eneo la mji wa Bwega wilayani hapa na kukuta mazingira ya eneo hilo yanateketea kwa moto leo asubuhi.
Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Col. Michael M. Ngayalina (katikati) akiwa na baadhi ya wananchi wenye mapenzi mema baada ya kushiriki zoezi la kuzima moto eneo la Bwega
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz