Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina ameipongeza Tanesco Wilaya ya Buhigwe kwa kushika nafasi ya kwanza kiwilaya katika utendaji wao wa kazi.
Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Tanesko Wilayani Buhigwe aliwapongeza na kuwahusia kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwahudumi Wananchi kwa weledi na kwa ushirikiano.
Naye Meneja wa Tanesco Wilaya ya Buhigwe Abdallah Mlamzi alisema kuwa wamepata ushindi huo baada ya kushindanishwa na Wilaya 134 na Mikoa 29 kwa kuzingatia vipengele tofautitofauti ikiwemo utoaji wa huduma,ushughulikiaji wa maombi ya wateja,ufanyaji wa Survey n.k ambazo zote walipata alama 100.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz