Mhe Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Col Michael Masala Justine Ngayalina akiwa kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyoadhimishwa katika kata ya Mkatanga wilayani humo ikiwa ni maadhimisho kiwilaya yaliyofanyika Tarehe 05/03/2023 Ametoa heshima kubwa sana ya dhati kwa wanawake wote Duniani kwani licha ya kuwa ni Jeshi kubwa pia ni nguzo kubwa katika Dunia
Ikumbukwe kuwa kauli mbiu ya siku ya wanawake Dunia mwaka 2024 Isemayo WEKEZA KWA WANAWAKE KUHARAKISHA MAENDELEO YA TAIFA KWA USTAWI WA JAMII Inatukumbusha kuwapa kipaumbele kikubwa wanawake katika uwekezaji ukizingati ndio mtaji mkubwa kwa jamii. Hatahivyo mhe DC amewatoa hofu wanawake wajasiriamali wote kuendelea kuchapa kazi kwani serikali ya mama SAMIA SULUHU HASSAN inapambana kwa juhudi zote ili kuwawezesha wanawake katika sekta zote za kiuchumi Kwani wanawake sasa ni viongozi wakubwa na ukizingatia Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania naye ni mama shupavu kweli kweli
Wakiwasilishwa taarifa yao kwa mhe DC wanawake wajasiriamali Wameomba serikali kuendelea kuwawezesha katika shughuli zao za ujasiriamali kwa kuwapatia mitaji na mafunzo ilihali hawajasahau kuomba kurejeshewa mikopo ya asilimia 4 ya wanawake ili kuendelea kukuza mitaji yao na kujipatia kipato .
Itoshe kusema kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Afisa Maendeleo ya Jami Ndug Christopher Kajange Ametoa shukurani zake za Dhati kwa wanawake wote kwa ushirikiano wao wa dhati waliouonesha kufanikisha zoezi hili na kuahidi kufanya zaidi na zaidi ili kuendelea kuthamini mchango wa wanawake katika jamii na ametoa shime kwa juhudi zao wanawake katika kulijenga Taifa La Tanzania
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz