Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Kanali Mstaafu Emmanuel Maganga ametoa vitambulisho 25,000 kuwatambua wafanyabiashara wadogo Mkoani Kigoma kuhakikisha wanafanya shughuli zao bila kusumbuliwa.
Rc ametoa vitambulisho hivyo leo Jumatano Desemba 19, 2018 kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari, Wakuu wa Wilaya zote Mkoani humo katika ukumbi wa mikutano Ofisini kwake na kujadili namna ya kuboresha mazingira ya ukusanyaji wa mapato.
Wilaya ya Buhigwe imepewa vitambulisho 2,000 na kila Mjasiriamali mdogo atalipa shilingi 20,000 kama ada ya kitambulisho kwa mwaka na fedha hiyo kupelekwa TRA.
Kwa malipo hayo Wilaya ya Buhigwe itakusanya shilingi milioni 4 na ikilazimu Mkuu wa Wilaya ataagiza vitambulisho vingine kwa ajili ya watakaovihitaji.
Mkuu wa Mkoa huo amewataka Wakuu wote wa Wilaya za mkoa wa Kigoma kuhakikisha wanagawa vitambulisho hivyo kwa Wajasiriamali na kufuatilia kwa karibu kuhakikisha Wajasiriamalii wote wenye sifa za kusajiliwa wanasajiliwa na kupata Vitambulisho vya Ujasiriamali kabla ya mwezi Januari 2019.
Zoezi la ugawaji Vitambulisho kwa Wajasiriamali wadogo mkoa wa Kigoma limehudhuriwa na Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Maafisa Biashara, Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, na vyombo vya habari; ambapo Waheshimiwa wakuu wa Wilaya walikabidhiwa Vitambulisho hivyo ili kuvigawa kwa Wajisiriamali wadogo katikla maeneo yao.
Mhe. Kanali Mstaafu Emmanuel Maganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma akimkabidhi vitambulisho vya wajasiriamali wadogo Mhe. Luteni Kanali Michael M. Ngayalina Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kwenye hafla ya uzinduzi wa kuanza kwa zoezi la ugawaji Vitambulisho vya Wajasiriamali wadogo kwa mkoa wa Kigoma.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz