Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Siro amewaasa Watumishi wa umma kutimiza Wajibu wao na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta maendeleo kwa Wananchi na taifa kwa ujumla.
Akizungumza na Watumishi,Wakuu wa Taasisi,Wazee Maarufu,Wafanyabiashara,Bodaboda na Wananchi wa Wilaya ya Buhigwe tarehe 11 Julai 2025 katika ziara yake ya kikazi wilayani humo amesema kuwa anatoa wito kwa Watumishi wote wa umma kutimiza wajibu wao bila kusubiri kusukumwa na mtu yoyote.
Aidha amewahimiza watumishi wa umma kuanza kuwekeza katika shughuli za uchumi na biashara wakiwa bado kazini badala ya kusubiri mafao ya kustaafu.
Sambamba na hilo ameongezea kwa kuwapongeza Wananchi wa Wilaya ya Buhigwe kwa mapokezi mazuri ambayo ameyapata alipotembelea katika Wilaya hiyo.
Licha ya hilo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuupatia Mkoa takribani Trilioni 11.4 katika bajeti ya mwaka 2023/2024.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz