Hayo yamesemwa na Mhe. ,Mkuu wa Mkoa Kigoma, Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye wakati wa ziara yake leo wilayani Buhigwe iliyolenga kuhamasisha Jamii juu ya Ulinzi wa Mwanamke na mtoto na Kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa. Ziara hii imefanyika katika kijiji cha Nyaruboza, kata ya Muhinda, Tarafa ya Manyovu.
Akizungumza na umati wa wananchi kijijini hapo, Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema, kulingana na utafiti, asilimia 60 ya ukatili dhidi ya watoto hutokea nyumbani na asilimia 50 hutokea shuleni ambapo wasababishi wa ukatili huo ni wazazi, walezi, ndugu na jamaa, walimu, watumishi wa shule na wanafunzi wenyewe.
Aidha unyanyasaji wa kingono; watoto 3 kati ya 10 wasichana, na mtoto 1 kati ya 7 wa kiume wamefanyiwa ukatili kabla hawajafikisha umri wa miaka 18. Unyanyasaji wa kimwili; asilimia 72 ya watoto wa kike na asilimia 71 ya watoto wa kiume wamefanyiwa ukatili kabla hawajafikisha umri wa miaka 18, Mtoto 1 kati ya 4 wamefanyiwa unyanyasaji wa kihisia kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.
Yapo maeneo 8 ya kimkakati ambayo yatatusaidia kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto; maeneo hayo ni pamoja na;
1. Kuimarisha Uchumi wa kaya
2. Mila na Destuli
3. Mazingira salama
4. Malezi, Kuimarisha mahusiano na kuziwezesha Familia
5. Utekelezaji na Usimamizi wa sheria
6. Utoaji wa Huduma kwa waathirika wa ukatili
7. Mazingira salama shuleni na stadi za maisha
8. Uratibu, Ufuatiliaji na Tathmini
Nawaagiza wazazi na walezi kuwaandikisha shule watoto wenye ulemavu ili wapate haki ya kuendelezwa, kupata elimu na kucheza na wenzao, kitendo cha kuwafungia ndani ni kinyume cha haki za binadamu.Tuondoe dhana potofu kwamba mtoto mwenye ulemavu ni ishara ya mikosi katika familia.
Kwa upande wa Mfuko wa Afya ulioboreshwa , Rc amesema zipo huduma nyingi zitolewazo kwa Mwanachama mwenye kadi ya CHF iliyoboreshwa ikiwemo; Ushauri wa Daktari, Vipimo vya maabara, Dawa, Uangalizi, Upasuaji, Huduma za kujifungua, Huduma za rufaa, Vipimo vya picha (x-rayna ultra sound), kulazwa. Huduma hizi zinatolewa kuanzia ngazin ya Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali ya wilaya na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Mhe. Mkuu wa Mkoa akitoa ofa ya kitambulisho cha Mfuko wa Bima ya Afya ulioboreshwa kwa Bi. Vaileth Kizanye.
Akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Dkt. Julius Nyasongo, amesema wananchi wanaendelea kujitokeza kujiunga na Mfuko wa CHF iliyoboreshwa na elimu ya kupinga ukatili dhidi ya mwanamke na mtoto inaendelea kutolewa kupitia kamati za MTAKUWWA ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji.
Dkt. Julius Nyasongo akisoma risala kwa Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Kigoma wakati wa ziara kijijini Nyaruboza tarehe 17/06/2021.
Kwa upande wake Mhe. Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Col. Michael M. Ngayalina alitoa ofa ya shilingi elfu tano kwa kila mwanachama mpya anayejiunga na CHF iliyoboreshwa kabla ya Mhe. Diwani wa katay hiyo kuhitimisha kwa kutoa ofa ya vitambulisho viwili vya mfuko wa CHF iliyoboreshwa.
Imetolewa na;
Idara ya TEHAMA,
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (w) Mji wa Bwega,
P.O.BOX 443
Buhigwe
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz