WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa Kassim(MB) leo tarehe 20 Julai 2024 amezindua rasmi uboreshaji wa daftari la wapiga kura lililofanyika katika viwanja vya Kakawa mkoani Kigoma na kuwataka watanzania wote kutimiza wajibu wao kwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura linaloendelea nchini.
Akizungumza katika uzinduzi huo amesema kuwa kila mtanzania ana wajibu wa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kutimiza wajibu wa mtanzania mzalendo. Sambamba na hilo ametoa rai kwa watendaji kutumia lugha nzuri na maelekezo thabiti kwa wananchi katika utekelezaji wa zoezi la uboreshaji ili kuhakikisha kila mtanzania mwenye sifa anapata nafasi ya kushiriki katika zoezi hilo.
Naye mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya uchaguzi Jaji Mwambegele amesema kuwa uboreshaji wa daftari la wapiga kura umeanza kwa awamu ya kwanza ambao utahusisha mizunguko 13 na kwa mikoa mitatu ambayo ni Kigoma,Tabora na Katavi.
Ameongezea kwa kusema kuwa Tume ina wajibu wa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kuramara mbili katika kipindi kinachoanza baada ya uchaguzi mkuu.
Aidha amesema kuwa kwa upande wa Zanzibar zoezi hili litafanyika kuanzia 7 mpaka 13 octoba 2024 Jumla ya vituo 40126 vitatumika katika zoezi la uboreshaji wa daftari na kati ya hivyo 39709 vipo Tanzania bara na vituo 417 vipo Tanzania Zanzibar ikiwa ni ongezeko la vituo 2312 zaidi ikiliinganishwa na vituo 37814 vilivyotumika katika zoezi la uandikishaji 2019/2020.
Sambamba na hilo amesema kuwa Tume imehuisha mifumo ya uandikishaji wa wapiga kura na kwa uboreshaji unaoanza leo kwa wananchi waliomo kwenye daftari wanaweza kuanzisha mchakato wa kuboresha au kuhamisha taarifa zao wakiwa nje ya kituo kwa njia ya kielectronic kwa kutumia simu ndogo maarufu kama kiswaswadu.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz