Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe na Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya,Ndug George Emmanuel Mbilinyi tarehe 27 mwezi Septemba amekutana na Viongozi wa Vyama vya Siasa wa wilayani humo kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Akizungumza katika kikao hicho aliwasihi kwa pamoja kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano kwa ajili ya ujenzi wa taifa moja la Tanzania.
Sambamba na hilo aliwasihi kusimamia na kufanya kampeni za kistaarabu pale muda utakapowadia.
Kwa niaba ya vyama vya Siasa Wilaya ya Buhigwe Katibu wa Chama cha CUF Dismas lilangeza alimpongeza Mkurugenzi kwa kuwaita kwa pamoja na kuwapatia Elimu ya Uchaguzi na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz