Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Mhe. Kanali Michael Ngayalina aliyevaa nguo za jeshi akishiriki na wananchi kupanga tanuru katika ujenzi wa kituo cha afya Kajana
sehemu ya watumishi wa halmashauri wakishiriki kufyatua tofali za ujezni wa kituo cha afya Kajana.
Katika kuhakikisha kuwa zoezi la ujenzi wa kituo cha Afya cha Kajana ambacho kimeletewa Tsh 500,000,000/= linaenda kwa kasi na kukamilika kwa wakati mkuu wa wilaya Mhe. Kanali Michael Ngayalina akishirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na wakuu wa idara wa halmashauri wametia hamasa kwa kushiriki kufyatua tofali na kupanga tanuru katika maandaliniz ya ujenzi wa kituo hicho leo Julai 29, 2021.
Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Mhe. Kanali Michael Ngayalina kushoto akiongea na wananchi baada ya kushiriki shughuli ya kufyatua tofali za ujenzi wa kituo cha afya Kajana
Serikali ya Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan imetoa Tsh milioni mia tano (500,000,000/=) kwa ajili ya kituo hicho cha afya.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz