Tarehe 24/12/2021 Wilayan ya Buhigwe ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Col. Michael Masala Ngayalina akiambatana na maafisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Buhigwe, Alitoa zawadi mbalimbali za Krismas kwa watoto 48 waliokuwa wakiishi katika mazingira hatarishi apo awali (Yatima, watoto waliotupwa, waliozaliwa na watu wenye matatizo ya afya ya akili, kutelekezwa na kufanyiwa ukatili). Aidha, kwa sasa kutokana na changamoto walizo nazo watoto hao, imewapelekea kuishi na kulelewa kituo cha Matyazo (Bethel children's Home) kilichopo Wilaya ya Kigoma Vijijini ambapo kituo hiki hupokea watoto kutoka Wilaya/Mikoa mbalimbali ikiwemo watoto 10 kutoka Wilaya ya Buhigwe. Pamoja na mambo mengine, katika kufika huko Mh. Makamu wa Rais Dr. Philip Isdor Mpango kupitia Mh. Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe alituma salaam za kuwatakia Kheri ya Krismas watoto hao, waangalizi wao pamoja na Wana-Buhigwe wote.
Kheri ya Krismas na Mwaka mpya.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz