MKURUGENZI MBILINYI ATEMBELEA WATUMISHI OFISI KWA OFISI
Posted on: April 18th, 2024
Awataka kujikita kwenye utoaji wa Huduma Bora na kwa wakati kwa wananchi
Upungufu wa Watumishi wamgusa na kuahidi kufanyia kazi changamoto hiyo
Ataka matumizi sahihi ya Fedha za Uendeshaji wa ofisi
Asisitiza Uwajibikaji na Uzalendo
Utunzaji wa mali za Serikali kuendelea
Atoa agizo kufikia Aprili 30 kuhamishwa kwa magari yote ya Halmashauri yaliyo nje ya Eneo kwenda ndani ya eneo ilipo Halmashauri ili kupunguza gharama za Ulinzi na kuongeza usalama
Ataka matengenezo yote ya Magari kukarabatiwa na kufanya kazi kufikia Mei 30, 2024
Aonya kutokuwepo ‘Mipango’ ubabaishaji katika matengenezo ya Magari na kutaka Vitengo na Divisheni kusimamia ‘maintanance’ ya magari kwa wakati
Akoshwa na utoaji wa Huduma kwa wagonjwa Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe na kuwataka watumishi kuendelea kuwafanya wananchi kuwa kipaumbele chao katika utoaji wa Huduma