Mhe. Col. Michael Ngayalina, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe ameongoza zoezi la upandaji miti kwenye eneo inapojengwa Shule Mpya ya Sekondari Biharu, katani Biharu Wilayani humo ambapo katika kutekeleza dhana ya utunzaji wa Mazingira Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kuridhisha tabia ya utunzaji mazingira kwa kizazi kijacho kwa kuwa kutunza mazingira ni kutunza Maisha
Mkurugenzi wa Programu ya Tuungane ambayo imejikita katika Utunzaji wa Mazingira kupitia Utunzaji na Upandaji Miti, Ndg. Lukindo Hiza ameshukuru namna ambavyo wananchi wameipokea Program hiyo na kuonesha Ushirikiano katika kufikia Lengo la Buhigwe ya Kijani yenye Uoto wa Asili.
Awali Ndg. Alphonce Haule, Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe amesema wameazimia kwenye Baraza la Madiwani kuwa kila Kata kuwa na Shamba la Miti ili kuenedeleza kuenzi dhana ya Utunzaji wa Mazingira kwa upandaji miti kwa Vitendo.
Ndg. Utefta Mahega, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo ameshukuru namna Zoezi na Program hiyo inavyoendeshwa ili kubadili Buhigwe ambayo uharibifu wa Mazingira nii Mkubwa hivyo kutishia kizazi cha sasa na kijacho.
Mhe. Felix Kavejuru, Mbunge wa Jimbo la Buhigwe akiwasilisha Salamu za Mhe Samia Suluhu Hassan, amewataka wananchi kutumia Mvua zinazoendelea kunyesha kulima kikamilifu ili kuepukana na majanga ya njaa ila wazitumie kuzalisha ili kupata Chakula cha kutosha na kujiongezea kipato kwao na kwa Halamshauri.
Kabla ya zoezi la Upandaji Miti kwenye eneo hilo, uongozi wa Wilaya walitembelea na kukagua vitalu vyenye miche Takribani Milioni 2 ya aina mbali mbali hasa yenye kulinda na kutunza maji ambapo vitalu hivyo vinatunzwa na kikundi cha Tuungane ambacho baada ya kukuza miti hiyo huigawa Bure kwa wananchi ili wapande kwenye maeneo yao Pamoja na taasisi.
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya hawakuwa nyuma kushiriki zoezi hilo ambapo kupitia Mwenyekiti wao Ndg. Erneo Dyagula wameshukuru namna ambavyo wananchi wameendelea kumuunga Mkono Mhe. Rais Samia kwa Vitendo na kuwataka waendelee kujitokeza kila shughuli ya Maendeleo inapofanyika ili kufikia Buhigwe inayotajwa na Ilani.
Wilaya ya Buhigwe ni miongoni mwa Wilaya zenye Mvua nyingi lakini kutokana na uharibifu wa Mazingira maeneo mengi yamebaki na nyasi fupi na vichaka tofauti na awali ambapo miti ya asili ilitamalaki kila mahali ambapo sasa Juhudi za makusudi za kila mmoja zinahitajika, akiongeza kwenye Hotuba yake Mhe Ngayalina amewasihi wananchi kuacha tabia ya Uchomaji holela wa Miti
Jumla ya Miti 1000 imepandwa kwenye eneo hilo kama ishara ya kuendelea kutia shime wananchi kuendeleza dhana ya Utunzaji wa mazingira kwa Upandaji Miti ambapo zoezi hilo limeongozwa na Mhe. Ngayalina ambaye amekuwa Kielelezo katika kuhakikisha dhana ya Utunzaji mazingira inafanywa kwa vitendo wilayani hapo ambapo kila mwaka wamedhamiria kupanda Miche mipya Takribani Milioni Mbili hadi Tatu
Program ya Tuungane inatekelezwa Wilayani Humo ikiwa na Jumla ya Vitalu Viwili Wilayani Humo vyenye Jumla ya Miche 2,080,000.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz