Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Justin Ngayalina leo tarehe 10 Novemba 2025 ameongoza zoezi la ugawaji wa Miche takribani 1,400,000 bure kwa Wakulima wa kata ya Kibwigwa, Mwayaya na Mkatanga iliyozalishwa na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kupitia kampuni ya B - PLUS.

Akizungumza na Wananchi hao, Mkuu wa Wilaya amewasihi kuilea na kuitunza vizuri miche hiyo ili kupata mavuno yatakayo wakwamua kiuchumi kwa kila mkulima lakini pia kuiendeleza Nchi kupitia sekta ya kilimo.

Aidha ameongezea kwa kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Makampuni yanayojihusisha na kilimo na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndug George Emmanuel Mbilinyi kwa uamuzi wa kuzalisha miche hiyo katika maeneo ya Halmashauri.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa katika wilaya ya Buhigwe wakulima wanaolima kahawa na waliosajiliwa ni 6,128 na eneo linalolimwa zao LA Kahawa ni Ekari 11,820, hivyo kupitia ugawaji wa miche hiyo itaongeza idadi ya Wakulima na eneo linalolimwa katika Wilaya ya Buhigwe.

Naye Alphonce I. Haule ambae ni Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Buhigwe amesema kuwa miche hiyo ya ruzuku inagawiwa bure kwa Wananchi ili kuhakikisha kila Mwananchi anapata kulingana na mahitaji ya shamba lake.
Kwa kumalizia Msimamizi wa kampuni ya B - PLUS amewapongeza AMCOS ya Kibwigwa ambao walitoa eneo hilo la ardhi kwa ajili ya kupandia miche hiyo na wote waliojitokeza kwa wingi kuja kupokea miche hiyo.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz