Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Canali. Michael M. Ngayaliani amefanya uzinduzi huu kwa wajumbe wa kamati ya Lishe Wilayani Buhigwe. Kupitia kamapeni hiyo wajumbe wote wa Wilaya walishiki kwa kuweka mazingatio yote juu ya kuondosha kabisa hali ya udumuvu wa watoto katika Wilaya ya Buhigwe.
Wajumbe wa kamati ya lishe walipia kwenye mafunzo hayo kwa kushirikiana na wajumbe kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi (OR-TAMISEMI). Katika mafunzo hayo wajumbe walifundishwa umuhimu wa siku 1000 ZA MTOTO.
Siku 1000 zinamaana hasa katika makuzi ya mtoto yeyeto. Kwa mchanganuo wa makundi matatu.
1. siku 270 za kwanza nisiku kuanzia siku ya utungaji mimba hadi kujifungua kwa Mama, na hapa mtoto akifikisha miezi sita (6) mtoto anahisi kila kitu kinachoendelea katika dunia, hasa ikiwa mabadiliko ya mama ya kimazingiza na kama anahasira na ogomzi wa kati ya Wazazi basi inapelekea mtoto kuhusi mabadiliko hayo kwenye mwili.
2. siku 365 za kwanza ni jumla ya umri wa mwaka mmoja kwa mtoto ambo mzazi anatakiwa kumjengea mtoto mazingira yote ya kujifunza kwakuwa kipindi hiki ndio chocho ukuwaji wa Ubongo wa mtoto unafanyika.
3. Siku 365 za pili nikipindi ambacho ukuwaji huu ndio unafanyika kwa kasi. na kama ikitokea makosa katika lishe, mazoezi changamfu basi hali ya mtoto itakuwa hivyo katika ukuwaji wake wote.
Kampeni hii ilienda kwa jina la "MTOTO MWEREVU NIJUKUMU LANGU".
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz