Awali ya yote Akizingumuza na wafanya kazi wa vyama vyote mgeni Rasmi Mhe. Cgf (Mst.) Thobias Andengenye amesema’’napenda kwanza niitumie fursa hii kuwashukuru kwa dhati, Viongozi wa Vyama huru vya Wafanyakazi chini ya uratibu wa TUCTA kwa uamuzi wao wa kunialika kuja kushiriki nanyi kama mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi au Mei Mosi, tukio ambalo husherehekewa kila mwaka katika kila Mkoa hapa nchini na ulimwenguni kote. Ninawashukuru na kuwapongeza sana kwa kunitunukia heshima hii ya pekee”
Akitoa pongezi na shukurani za dhati amesema”Kwa dhati ya moyo wangu napenda kuchukua fursa hii kumpongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa ambazo amezifanya na anazoendelea kuzichukua katika kuondoa kero mbalimbali za wafanyakazi nchini Tanzania. Hii inadhihirisha dhamira na nia njema ya Rais wetu katika kuthamini mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya Taifa letu
.
Aidha Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu ni “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha” kauli mbiu hii inaakisi kabisa chimbuko na historia ya sikukuu ya Mei Mosi.
Akieleza kuhusu changamoto zilizowasilisha kwenye risala amesema” Katika risala yenu mmegusia kero mbalimbali zinazowahusu wafanyakazi wa Serikali, Mashirika, na wale wa sekta binafsi hasa tatizo la mikataba. Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano unaostahili kwa vyama vya wafanyakazi na wadau wengine wanaoshughulikia haki za wafanyakazi katika kuhakikisha kuwa sheria mpya za kazi Na. 6 na Na.7 zinatekelezwa ipasavyo. Kwa kufanya hivyo matatizo mengi yatapungua kama sio kumalizika kabisa. Napenda kuchukua fursa hii kuwaasa waajiri wanaowanyanyasa na kuwakandamiza wafanyakazi wao kwa namna yoyote ile waache kufanya hivyo. Nawataka wafuate sheria mpya za kazi katika kuajiri na kutekeleza haki na wajibu wa wafanyakazi. Aidha vyama vya wafanyakazi visaidie kuwabaini waajiri wa namna hii ili wapelekwe kwenye mkondo wa sheria. Hata hivyo kama nilivyosema hapo awali wafanyakazi nao wanapaswa kutekeleza wajibu wao ipasavyo mahali popote pa kazi.”
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz