Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Wilaya ya Buhigwe,ikiongozwa na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mh Diwani Robson Mzimya,leo tarehe 05 Novemba 2024 imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali.
Miradi hiyo ikiwemo Ujenzi wa Chumba kimoja cha darasa na matundu 08 ya vyoo Bwafumba Sekondari wenye thamani ya shilingi Mil 39,400,000.Ujenzi wa shule mpya yenye vyumba 09 vya madarasa S/Msingi Kamanga wenye thamani ya shiling Mil 364,500,000 Ujenzi wa darasa 01 na matundu 08 ya vyoo Kafunya Sekondari shilingi Mil39,400,000 na Ujenzi wa nyumba ya mtumishi katika kituo cha Afisa Ugani Kibwigwa shil Mil40,000,000.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz