Aliyasema hayo jana,kaimu Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Isaac Mwakisu katika kongamano la uwasilishaji wa taarifa ya robo ya mwaka ya utendaji kazi wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
“Mashirika yote yanatakiwa kufuata masharti,sheria na taratibu za Nchi ikiwemo kufanya kazi kwa mujibu wa Nyaraka za usajili na katiba,kuhakikisha inalinda maslahi ya Nchi,kutiii na kulinda utamaduni,kuwasilisha taarifa kwa Halmashauri,”alisema Mwakisu
Aliongezea kwa kusema kuwa Serikali haitomuonea huruma yeyote ambaye hatafuata sheria za Nchi kwa kigezo cha kuleta maendeleo na haitosita kumchukulia hatua za kisheria pale tu atakapogundulika kukiuka sheria hizo.
Sambamba na hilo aliwataka kuzingatia mila na desturi za Nchi,uwazi na uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi.
Kwa upande wake katibu tawala wa Wilaya hiyo Bi Utefta Mahega alisema kuwa kongamano hilo limefanyika likiwa na lengo la kuongeza chachu na ushirikiano wa utendaji kazi wa mashirika hayo na serikali.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Bi Emmily Fwambo aliwataka watumishi wa Mashirika hayo kuweka utu mbele kuliko fedha.
“Kama watanzania tuzingatie maadili tusimame na kuwasaidia watu wetu na tusidanganywe na misaada tunayopewa na wafadhili tuwe na utu na ubinadamu”alisema Fwambo
Kongamano hilo limefanyika likiwa na Kaulimbiu inayosema “Mashirika yasiyo ya kiserikali ni wadau muhimu washirikishwe katika utawala bora”
Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ina jumla ya Mashirika 19 yasiyokuwa ya kiserikali yanayo fanya kazi katika sekta za Elimu , Kilimo , Afya, Mazingira , Utoaji wa elimu ya Mapambano dhidi ya Ukatili.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz