Akizungumza Mwakilishi wa katibu tawala mkoa na msimamizi wa Serikali za mitaa Bi Dorothea Lugwangara katika kikao jumuishi cha Ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mwanamke na Mtoto(MTAKUWWA)ngazi ya Mkoa kufuatilia utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika Halmashauri ya Wilaya Buhigwe.
Alielekeza kuwa, kesi zote zinazofika ofisi za Ustawi wa Jamii na madawati ya jinsia yanayohusu matukio ya ubakaji hayatakiwi kusuluhishwa kwa namna yoyote.
Naye polisi kitengo cha dawati la jinsia na watoto ngazi mkoa Inspekta Michael Mjema ameipongeza ofisi ya Ustawi wa Jamii,Dawati la Jinsia Wilaya ya Buhigwe kwa taarifa iliyotolewa pamoja na utendaji kazi wao mzuri na ushirikiano uliopo baina yao.
“Niwapongeze kwa kazi mnazozifanya ambazo ni kubwa na nzuri pamoja na ushirikiano mzuri uliopo baina yenu ambao unawawezesha kutimiza wajibu na pia msife moyo katika kuwasaidia wananchi”Alisisitiza Mjema.
Katika taarifa iliyotolewa na Clement Ndangika Afisa ustawi wa jamii Wilaya ya Buhigwe alisema kuwa Halmashauri ya Wilaya Buhigwe ni miongoni mwa Halmashauri nane za mkoa wa Kigoma zinazosimamia na kutekeleza viashiria vya ulinzi na usalama wa mwanamke na mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili.
Aidha alielezea juu ya uwepo wa vitendo vya ukatili na kisha kuongeza kuwa,eneo la kukemea ukatili lapaswa kuwa la kila mmoja katika jamii ili kuhakikisha tunazuia isitokee lakini pia ikitokea tutoe taarifa mapema ili kumtia hatiani mtenda na kumsaidia manusura wa ukatili kupata huduma (mfano,dawa kinga) na msaada wa kisaikolojia kabla ya madhara makubwa yanayoweza kujitokeza baada ya tukio
Na kuongezea kuwa Utekelezaji huo ni sehemu ya mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) wa mwaka 2017/2018-2021/2022.
Naye Honorina Herman (Familia ya kuaminika) alisema kuwa ana upendo wa dhati kwa watoto wote na hiyo ndiyo sababu ya yeye kujitolea kuwahudumia watoto ambao wametendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz