Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Mohamed O. Mchengerwa siku ya tarehe 23/5/2025 amefungua kikao kazi cha Maafisa habari wa Halmashauri, Mikoa na taasisi zilizopo chini ya wizara yake.
Akizungumza katika kikao hicho amewataka Maafisa habari kutumia vizuri mamlaka waliopewa na Serikali kwa ajili ya kutangaza miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Mmebeba dhamana kubwa ya kuhakikisha mnatangaza miradi ya maendeleo katika taasisi zenu na mtumie fursa hiyo kuhakikisha wananchi wanapata habari na habari zilizo sahihi hivyo msiwaache watanzania
walishwe habari potofu”Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Kikao kazi cha Maafisa habari kinafanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Jiji Dodoma, na baada ya kikao kazi, Maafisa watatembelea na kuona miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Mkoa wa Dodoma.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz