Katibu Tawala wilaya ya Buhigwe Ndg. Peter Masindi amesema vitendo vya udumavu kwa watoto unaotokana na unyonyeshaji hafifu na lishe duni haukubaliki na kwamba "mtoto mwerevu ni jukumu langu".
Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Buhigwe kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika katika viunga vya shule ya msingi Buhigwe leo majira ya saa 9 alasiri Masindi amesema kumnyonyesha mtoto siyo jukumu la mama peke yake bali familia nzima. Ni lazima wazazi washirikiane kuhakikisha mtoto ananyonya maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo bila kulishwa au kunyweshwa kitu chochote, mtoto anyonye maziwa ya mama kwa muda usiopungua miaka miwili.
Kwa upande wake Afisa Lishe (w) Bi. Catherine Masawe amesema kuna faida nyingi sana za unyonyeshaji kwa mama, mtoto na familia kwa ujumla. Nawasisitiza akina mama wa Wilaya ya Buhigwe kunyonyesha watoto ili kuwakinga watoto dhidi ya magonjwa mbalimbali kama kuhara, utapiamlo, kupungua uzito, udumavu na hata vifo, pia faida kwa akina mama ni pamoja na kutokupata hedhi na hivyo kuzuia mimba kwa kipindi cha miezi 6 ya mwanzo, kuepuka magonjwa ya kuvimba chuchu au matiti, na kupunguza uwezekano wa kupata fistula. Alisema Catherine.
Aidha maziwa ya mama ya njano ni muhimu sana kwa afya ya mtoto, baadhi ya akina mama huyakamulia chini kwamba ni machafu kitu ambacho ni imani potofu inayopaswa kupigwa vita. Hakuna mama ambaye maziwa yake ni machafu, maziwa ya mama yoyote yana virutubisho sawa tuache dhana potofu tubadilike. Alimalizia Catherine.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz