Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina amesema ili kufikia malengo ya kiutendaji yaliyowekwa na serikali, watumishi wa Umma wanapaswa kupendana, kuheshimiana na kuwa wamoja ndani na nje ya maeneo yao ya kazi.
Kanali Ngayalina ametoa nasaha hizo alipozungumza wakati akifungua hafla fupi ya kuuaga Mwaka 2023 na kuukaribisha 2024 iliyofanyika 16 February 2024 katika Ukumbi wa Shambani Village Park wilayani Buhigwe iliyolenga kuwakutanisha pamoja watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
"Tunapokutana kama hivi inaongeza ukaribu kwa watumishi, kutambuana, kubadilishana mawazo sambamba na kuondoa msongo wa mawazo, niwasihi utaratibu huu uendelee kwani unatupatia fursa ya kukutana nje ya maeneo ya kazi na kujenga ukaribu na kuimarisha mahusiano ya kiutumishi baina yetu" alisisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.
Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.ndugu Alphonce I Haule.amesema watumishi wa Umma wanapaswa kuwa na ushirikiano ndani na nje ya maeneo yao ya kazi jambo linaloimarisha utendaji kazi wao na kuleta matokeo chanya katika utoaji huduma kwa jamii.
Aidha Mkurugenzi huyo amewataka watumishi hao kuboresha utendaji kazi wao kwa mwaka 2024 kwa kuutumia Mwaka 2023 kama darasa ili kuondoa mapungufu yaliyojitokeza.
Upande wake Katibu Tawala wa Halmashauri wa wilaya hiyo Bi. Utefuta Mahega....amewasisitiza watumishi hao kuimarisha ushirikiano na kuongeza kasi katika kuwahudumia wananchi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz