Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe Anosta Lazaro Nyamoga amezindua rasmi mnada wa mifugo, bidhaa za viwandani na mashambani wilayani Buhigwe.
Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatano 10-03-2021 katika kijiji cha Kavomo kilichopo kata ya Buhigwe mkoani Kigoma barabara ya Kasulu-Munanila.
Nyamoga amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wakulima, wafugaji na wafanyabiashara wanalipwa fedha na kuuza mifugo na mazao yao kwa bei nzuri hivyo anaamini Mnada huo utasaidia wakulima na wafugaji kuuza bidhaa zao kwa bei elekezi. Hivyo nawaasa
-Wananchi kujituma katika kufanya kazi kwa bidii siku zote ili kujiletea maendeleo ya mtu binafsi, kaya na Taifa kwa ujumla
- Kila mfanyabiashara kutumia busara katika kufanya biashara hapa mnadani bila kuanzisha tabia mbaya za vurugu, wizi navingine vinavyofanana na hivi ili kuinua hali ya kibiashara ambayo itatunufaisha sisi sote.
- Kila mtu aliyefika hapa leo awe mwakilishi mzuri wa kuutangaza mnada huu ndani na nje ya Wilaya ya Buhigwe ili uendelee kukua.
Mnada utakuwa unafanyika kila Jumatano ya wiki na bidhaa mbalimbali zitauzwa na kununuliwa; Mifugo (Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo, Kanga, Kuku wa kienyeji wapo kwa wingi), mazao (Michikichi, Mahindi, Alizeti, Mbaazi, Mtama na Ulezi), Matunda, bidhaa mbalimbali za madukani zinapatikana kwa uhalisia wa gharama utakayoimudu.
Kwa kuhitimisha Nyamoga alisema lengo la kuwepo kwa mnada huo ni pamoja na;
kuongeza wigo wa eneo la watu wengi kuweza kufanya biashara,
Kuweka msingi wa kuimarisha masoko ya uchumi wa viwanda utakaokuwa na bidhaa nyingi.
Faida za Kuwepo kwa Mnada huu
Kuongeza ajira katika jamii yetu kupitia kushiriki katika biashara na utoaji huduma mbalimbali,
Kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na familia kwa ujumla.
Kurahisisha upatikanaji wa vyakula na huduma zingine muhimu.
Kwa ujumla wake yote haya husababisha mwananchi kujikwamua kutoka kwenye wimbi la umasikini na kujiongezea kipato
Nyama choma ya Mbuzi mnadani
Biashara ya nguo katika mnada wa Buhigwe
Vyombo mbalimbali kwa matumizi ya nyumbani
Karibu Buhigwe, karibu Mnada Mpya wa Buhigwe kila Jumatano ya wiki.
Imetolewa na;
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
Buhigwe.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz