Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buhigwe Ndg George E Mbilinyi leo Mei 31,2024 amefanya uzinduzi wa zoezi la kugawa dawa za kuogeshea mifugo au ng’ombe.
Zoezi hilo limefanyika katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ambapo amewakabidhi dawa viongozi walio wawakilisha wafugaji wa kata zote za Halmashauri ya Buhigwe.
Mbilinyi amesema kuwa Dhamira ya serikali ni kuona wafugaji wanafuga mifugo yenye Afya njema kwasababu ukiogesha mifugo unaenda kutibu magonjwa ambayo yanasumbua mifugo hiyo.
Serikali imeonesha mfano wa namna bora ya kutunza au kufuga mifugo ndiyo maana imewaleta wataalamu wa mifugo ili tuweze kupata usaidizi wa karibu wa fuga na pia wataalamu wa kilimo ili kuhakikisha wakulima nao wanalima kilimo chenye tija.
Sambamba na hayo pia Viongozi wa wafugaji waliofika katika uzinduzi huo wamemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuwakumbuka na kuwapatia ruzuku hiyo ya dawa kwaajili ya kutibu mifugo yao kitu ambacho wao kinawapa shinda kutimiza katika mahitaji yao ya ufugaji bora.
Wakati hayo yakiendelea Mbilinyi amepata wasaa wa kuzungumza na watumishi wa Idara ya kilimo ngazi zote za Halmashauri kwa lengo la kusikiliza malalamiko na kero zao hatimaye kuzipatia ufumbuzi.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz