Ndg. George Mbilinyi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Buhigwe Leo Aprili 15, amefanya kikao kazi na watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe baada ya kuanza kazi Rasmi ambapo ametoa Dira ya mabadiliko ya Utendaji katika kipindi cha Uongozi wake.
Awali aliyekuwa kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Alphonce Haule amewashukuru watumishi kwa namna walivyoshirikiana kwa kipindi cha Miezi nane aliyokuwa akikaimu na kuwataka kuonesha ushirikiano kwa Mkurugenzi mpya.
Akiongea kwa msisitizo Mkurugenzi Mtendaji George Mbilinyi amesisitiza Uzalendo katika kuwatumikia watumishi na kuonya watakaojifanya Miungu watu na wenye Viburi katika kutumikia wananchi. Awali wakati wa kuongea alimshuruku Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa JMT kwa kuendelea kumuamini kumsaidia kuwatumikia wananchi wa Buhigwe
Akishukuru na kumkaribisha kwa niaba ya Watumishi wengine Ndg. Masau Koligo ameonesha matumaini makubwa katika uongozi mpya na kumhakikishia ushirikiano mkubwa.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz