Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndugu George Emmanuel Mbilinyi amewaasa Wananchi kutunza miradi ambayo inaletwa na Serikali kwa faida ya kizazi cha leo na kesho.
Ameyasema hayo leo tarehe 26 mwezi wa pili mwaka 2024 katika makabidhiano ya madarasa matatu yaliyojengwa katika Shule ya msingi Chagwe kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Aidha ameongezea kwa Kuwaasa Wazazi na Walezi kuhakikisha wanawezesha zoezi la upatikanaji wa chakula kwa Wanafunzi Shuleni.
Kwa upande wake Afisa Mradi kutoka (TEA) Paul Kawawa amewapongeza Walimu,Wanafunzi na Wazazi kwa kutunza mazingira ya madarasa hayo tangu mradi ulipoanza mpaka ulipomalizika.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule hyo Limwengu Mwamba amesema kuwa shule ilipokea shilingi Milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa.
Sambamba na hilo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuleta miradi mbalimbali ya Elimu Tanzania.
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz