Katika kuadhimisha kilele cha Miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika Wilaya ya Buhigwe imefanya zoezi la upandaji wa miti kata ya Janda,Kijiji cha Kirungu kwenye eneo la ujenzi wa shule ya Sekondari mpya ya Kirungu.
Akizungumza na Wananchi baada ya kumalizika kwa zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina amesema kuwa katika kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Tanganyika kama Wilaya imefanya shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya usafi,kupanda miti katika maeneo mbalimbali ili kuenzi juhudi za wapigania Uhuru na kutimiza malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu ya kulinda Mazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Ndug George E,Mbilinyi amewashukuru wote walioshiriki katika zoezi hilo pamoja na kuwahusia Wananchi kutunza miti hiyo.
Naye Helleni Dalali Mkuu wa kitengo cha Mazingira na Jamii katika bank ya Equity amewashukuru viongozi wa Wilaya ikiwemo Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji kwa ushirikiano pamoja na kuwaasa Wananchi wote kutunza Mazingira na kuendelea kupanda miti katika maeneo mengine.
Miche hiyo iliyopandwa katika Shule mpya ni jumla ya miche 10,0000 iliyoletwa na Equity bank kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS).
Mji Mpya wa Bwega-Ofisi za Mkurugenzi
Postal Address: P.O.Box 443 Buhigwe
Simu Ya Mezani: 0282988460
Simu ya mkononi: (+255) 782 500 333
Barua Pepe: ded@buhigwedc.go.tz